PUNGUZA UVUMI ADAI TUJU
Written by Inka FM on 22 July 2021
Katibu mkuu wa chama cha jubilee Raphael Tuju amepuuzilia mbali madai kuwa kuna uwezekano wa chama cha jubilee kuunga na chama cha ODM katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza Jumatano usiku katika kituo kimoja cha televisheni nchini ,katibu mkuu huyo wa chama kinachotawala alisema kilicho kati ya vyama hivyo ni mkataba wa maelewano wa kufanya kazi pamoja na ndio sababu cha ODM kimeunga mkono jubilee bungeni na sekta zingine kimaendeleo.
Aliendelea kusema kuwa,’’chama anachoongoza Raila Odinga ni rafiki na hivyo watu waache dhana zao potovu, kama watu wanaongea kirafiki tunawaambia tusaidiane hapa,mswada huu unakuja na tunahitaji idadi fulani kuupitisha wanafanya adabu kutusaidia.Tukiketi chini na wenzetu ambao wametupa msaada asilimia mia bungeni,watu wanaanzakuongea kuhusu muungano.Hawaelewi neno muungano na hakuna mungano ilatu mkataba wa maelewano.”
Tuju alisema kinachoendelea kati yao ni uhusiano wakikazi na sio wa kisiasa“Tuna mkataba na Wiper tukakubaliana kuwa tutashirikiana katika maeneo Fulani, hayo ni makubaliani ya kazi na watu waache uvumi”.
Madai ya muungano wa jubilee na ODM yalienea kufuatia kukutana kwa viongozi kutoka vyama hivi kufanya mikutano na kukisiwa kuwa ni kuunda tunapokaribia uchaguzi mkuu mwaka ujao.Haya yanatukia siku chache tu wakati ambapo katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna amenukuliwa na madai kwamba wanaondoka katika muungano wa NASA ilikutafuta mwafaka na wenzao wa Jubilee.
Na John M.